POWA255's avatar
POWA255
npub1zkkl...6uwq
POWA 255 ni mpango wa elimu ya Bitcoin kwa njia ya mtu kwa mtu (peer-to-peer) unaolenga kusambaza maarifa ya Bitcoin kwa kutumia lugha ya Kiswahili.
POWA255's avatar
POWA255 5 hours ago
🎓 TREZOR ACADEMY – TANZANIA 🇹🇿 Bitcoin Education • Self-Custody • Security 🌍 #TrezorAcademy iko katika nchi 28 duniani ✨ Tanzania ni mojawapo! 📅 Mwezi wa Pili (Februari 2026) Bitcoin Arusha kwa kushirikiana na Powa 255 itaandaa muendelezo wa vipindi 3 vya Trezor Academy: 🗓 Tarehe: • 14 Februari-BITCOIN NI NINI • 21 Februari-MATUMIZI YA BITCOIN • 28 Februari- WATUMIAJI WENGINE WA BITCOIN WANAFANYA NINI? 📍 Mahali: Bitcoin Arusha Hub Jengo la Mega Complex floor ya Saba/WSHA Co-working space 📝 Jisajiri hapa kwaajiri ya session ya kwanza, Usajiri wa Session ya pili na ya tatu zitafata baada ya session ya kwanza kufanyika 🏅 Vyeti (Certificates) 🎁 Zawadi mbalimbali Zitatolewa kwa washiriki watakaohudhuria vipindi vyote vitatu kikamilifu 🤝 Imeandaliwa na: Powa255 x Bitcoin Arusha × Trezor Academy image
POWA255's avatar
POWA255 2 weeks ago
Tarehe 23/01/2026, POWA 255 na @Bitcoin Arusha kwa kushirikiana na @Hedhi Huru | Reusable Pads and Bitcoin Education walifanikisha mpango wa Reusable Menstrual Pads. Katika mpango huu, pedi zinazoweza kutumika tena zilitengenezwa na kugawiwa kwa wanafunzi takribani 42 wa Shule ya Sekondari Manushi, iliyopo Moshi, mkoa wa Kilimanjaro. ♻️📦 Pedi hizi zitawasaidia wanafunzi kuendelea kukaa shuleni kipindi chote cha hedhi kwa hadi miaka mitatu, bila vikwazo wala kukosa masomo. 🤝 Wewe pia unaweza kuwa sehemu ya mabadiliko haya Support kwa kumnunulia mwanafunzi mfuko mmoja wa pedi kupitia @Geyser
POWA255's avatar
POWA255 3 weeks ago
Tunafuraha kuwatangazia kuwa tumepokea vitabu viwili vya “THE BITCOIN STANDARD” vilivyotafsiriwa kwa lugha ya kiswahili kutoka Nairobi Kenya🇰🇪 Shukrani za dhati kwa exonumia.africa kwa kazi yao kubwa ya kutafsiri na kuifanya elimu ya #Bitcoin ipatikane kwa urahisi zaidi na kuwawezesha watu wengi kujifunza kwa lugha yao mama. Nakala moja ya vitabu hivi itatolewa shuleni ili kusaidia elimu na uelewa wa maswala ya fedha. Nakala nyingine itabaki katika hub ya @Bitcoin Arusha kwajili ya jamii kusoma, kujifunza na kukua pamoja. Hii ni hatua kubwa kuelekea kusambaza elimu ya #bitcoin Tanzania na barani Africa kwa ujumla. #BitcoinNiHela #bitcoinforeveryone
POWA255's avatar
POWA255 1 month ago
@manlikekweks akiwa ndani ya @Bitcoin Arusha Hub hapa WSHA Co-working space Akiwa amevalia T-shirt yetu Spesho ya #BitcoinNiHela🧡 Hi ni zaidi ya style ni ujumbe wa mabadiriko ya kifedha! Karibu utumbelee hub yetu ujifunze kuhusu #Bitcoin, uhuru wa kifedha na mengi zaidi 📍Mega Complex floor ya Saba (WSHA CO-working space). #bitcoinniHela #BitcoinArusha⚡️🧡 #POWA255⚡️ image