Habari za leo!
Juzi nchini Mauritius 🇲🇺 ilifanyika siku ya kwanza ya Btrust.tech Developer Day, tukio kubwa linalofanyika kila mwaka sambamba na Africa Bitcoin Conference. Hiki ni kipindi ambacho vijana, wabunifu na bitcoiners kutoka mataifa mbalimbali ya Afrika hukutana kwa ajili ya kujadili maendeleo ya teknolojia ya Bitcoin, fursa zilizopo na namna ya kukuza uelewa kwa jamii.
Katika Btrust Developer Day ya jana, tulishuhudia developers kutoka kona mbalimbali za bara hili wakijadiliana jinsi ya kujenga miradi juu ya Bitcoin open source, kuchangia maendeleo ya mfumo huu wa kifedha wa kidijitali na kusaidia jamii zao kufaidika kupitia teknolojia hii ya mabadiliko.
Bitcoin na teknolojia ya blockchain inaendelea kukua kwa kasi kubwa barani Afrika. Mataifa kama Nigeria, Kenya, Ghana, South Africa, Malawi, Burundi na Zambia yapo mbele sana katika kukuza matumizi ya Bitcoin. Tanzania 🇹🇿 bado ipo nyuma lakini tuna nafasi kubwa ya kufika mbali tukiamua kushirikiana.
Ni wakati wa vijana wa Tanzania kuamka, kushirikiana, na kujenga tech community imara. Tukiwekeza kwenye elimu, mafunzo, na ushirikiano, tunaweza kuinua taifa letu kwenye ramani ya kidijitali ya Afrika. Fursa zipo — tuzichangamkie!
https://blossom.primal.net/22b7c51744e16beb6b924cb7029852efdd1dd7440c26426c791720ce05c315dc.mp4
https://blossom.primal.net/4c5aed680421e155a6e187703ac5b8575b3152d2f65a198e10961051729e50b4.mp4
https://blossom.primal.net/22b7c51744e16beb6b924cb7029852efdd1dd7440c26426c791720ce05c315dc.mp4
https://blossom.primal.net/4c5aed680421e155a6e187703ac5b8575b3152d2f65a198e10961051729e50b4.mp4