Katika sekta ya Bitcoin & blockchain technology hapa Tanzania, vijana wa kiume wameonekana kuwa wengi na wenye uelewa mkubwa zaidi kuliko mabinti. Hii haimaanishi mabinti hawawezi, bali ni wito kwao kuamka na kuchukua nafasi zao katika teknolojia hii mpya inayobadilisha dunia. Ni muda wa akina dada wa Kitanzania kuamka na kujifunza zaidi kuhusu Bitcoin, blockchain, na fursa lukuki zilizopo. Karibuni kwenye Bitcoin Sister Hub Tanzania kupitia WhatsApp group, ambapo utapata elimu ya kina bure kabisa na kwa uelewa mzuri kutoka kwa jamii za tech za akina dada kama BitcoinDada, DadaDevs, Web3Ladies Club, na nyinginezo. Mabinti wengi wa Kenya na nchi nyingine wameingia kwa nguvu na wanafanya makubwa katika hii industry. Hii iwe chachu kwa mabinti wa Tanzania kuanza kujifunza, kushirikiana, na kuleta mabadiliko. Kama wewe ni mwanadada au mwanamama na ungependa kujifunza zaidi, tafadhali comment "naomba link ya group" na nitakutumia. Tuige mfano wa Madam Sandra (Mama Blockchain Tz) ambaye anajitahidi sana kueneza elimu ya blockchain kwa wanawake Tanzania. Teknolojia inasonga mbele — wadada muamke sasa!