Thread

Zero-JS Hypermedia Browser

Relays: 5
Replies: 0
Generated: 17:33:53
Btrust.tech ni jukwaa la kielimu linalolenga kukuza uelewa na ujuzi wa vijana wa Kiafrika kwenye teknolojia ya Bitcoin na blockchain , hususani kwenye maeneo ya Lightning Network development na open-source contributions. Kupitia programu zao, vijana—hasa developers —wanafundishwa kwa vitendo namna ya kuchangia miradi ya wazi, kujenga bidhaa bora za Bitcoin na kuwa sehemu ya mabadiliko ya kifedha ya dunia. Vijana wa Tanzania 🇹🇿 tunapaswa kuamka sasa! Dunia inabadilika kwa kasi, na blockchain ni mwelekeo mpya wa maendeleo ya kidigitali. Wakati wenzetu wa Nigeria, Ghana, Kenya, Uganda, Zambia na kwingine wakishirikiana, kujifunza na kukuza teknolojia hii, sisi bado wengi hatuwekezi muda kwenye elimu sahihi. Btrust.tech inatufungulia mlango wa fursa—tunapaswa kujiunga, kushirikiana na kusaidiana. Tukiungana kama vijana wa Tanzania katika kujifunza, kushiriki na kuboresha maarifa yetu ya blockchain, tunaweza kuleta mabadiliko makubwa kwenye jamii zetu. Fursa zipo—tuchukue hatua sasa! Tuache uzembe na dhana ya kujua kila kitu, tuchague kujifunza zaidi, kuungana na kuinua taifa letu kiteknolojia. Tukiwa pamoja, tutaifikia dunia! image image
2025-12-04 08:17:07 from 1 relay(s)
Login to reply